NYOTA YANGA AFIWA, WAMTOLEA RUTA UBANI WA MIL.1.5


BEKI wa klabu ya Yanga Chacha Marwa amefiwa na mtoto wake hivyo amelazimika kurejea jijini Dar es Salaam ili kuungana na wanafamilia katika msiba huo.
 Aidha,  mamia ya watu wakiwemo wanamichezo jana walijitokeza katika kanisa katoliki parokia ya Mtoni Kijichi kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga, Wakili Theonest Rutashoborwa.
 Rutashoborwa ambaye alikuwa akimiliki kampuni  ya Brilliance Law Chambers ya jijijini Dar es Salaam alifariki  usiku wa kuamkia Ijumaa katika hospitali ya Aga Khan kutokana na kuugua shinikizo la damu na kisukari anatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Bukabaye kilicopo Bukoba mkoani Kagera. 
Aidha uongozi wa Yanga kupitia Mwenyekiti wake Lloyd Nchunga umeelezwa kusikitishwa na kifo cha marehemu ambaye aliweza kuunganisha Wanayanga ambapo klabu hiyo ilitoa ubani wa shilingi mil.1.5.

Comments