NI BAYERN MUNICH NA CHELSEA FAINALI

Schweinsteiger
BAYERN Munich imeitoa Real Madird katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku huu na sasa itakutana na Chelsea katika fainali kwenye Uwanja wa nyumbani, Munich. Bayern wameitoa Real kwa penalti 3-2, kufuatia sare ya jumla ya 3-3, baada ya kila timu kushinda 2-1 nyumbani kwake. Mchezo wa leo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, wachezaji ghali wa Real, Ronaldo na Kaka walikosa penalti mbili za kwanza, baadaye Casillas akarejesha matumaini kwa kupangua penalti mbili mfululizo, lakini Sergio Ramos akakosa na Schweinsteiger akafunga ya mwisho na kuzima ndoto za Real kutwaa taji la 10 la Ligi ya Mabingwa.    

PENALTI ZILIVYOKUWA...
SCHWEINSTEIGER ANAFUNGA YA USHINDI!!!!!!! Kwa kujiamini kabisa anampoteza maboya Casillas, mpira unatinga nyavuni.
Schweinsteiger anakwenda kupiga akifunga, Bayern inaingia fainali...
NOMA, RAMOS!!! Anapiga shuti kali lakini mpira unapaa juu ya lango.
PENALTI YA LAHM INAOKOLEWA NA CASILLAS!! Alipiga shuti la kima cha mbuzi, na kwa urahisi Casillas akapangua!
ALONSO ANAFUNGA!!! Penalti hii inarejesha matumaini Real, alipiga shuti la kima cha mbuzi moja kwa moja.
CASILLAS NAOKOA PENALTI YA KROOS!!! Kipa wa Hispania anachumpa upande wake wa kushoto kupangua penalti ya Kroos.
PENALTI YA KAKA INAOKOLEWA!!! Neuer anasogea vizuri kuzuia shuti la Mbrazil huyo.
GOMEZ ANAFUNGA!!! 2-0 BAYERN!! inatinga nyavuni pembeni mwa lango.
NEUER ANAOKOA PENALTI YA RONALDO!! Kipa wa Ujerumani alifanya jitihada za hali ya juu kuokoa mkwaju uliolekezwa pembezoni kabisa mwa lango kulia kwake.
ALABA ANAFUNGA!!! Kinda huyo anatulia na kumtungua vizuri Casillas .


SOURCE: www.bongostaz.blogspot.com

Comments