NGORONGORO HEROES YAINGIA KAMBINI

Kocha Kim Poulsen, leo (Aprili 10 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa umri huo.
Kikosi hicho kimeingia kambini leo (Aprili 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi ya Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho ni Saleh Ally Malande (Simba), Aishi Salum Manula (Azam), Hassan Khamis Kessy (Mtibwa Sugar), Said Ruhava Samir (Falcon, Pemba), Carlos Protus Kilenge (TSC Mwanza), Dizzana Issa Yarouk (Azam), Amani Peter Kyata (African Lyon) na Issa Rashid Issa (Mtibwa Sugar).
Emily Mgeta Josiah (TSC Mwanza), Khamis Jamal Mroki (Mtibwa Sugar), Ramadhan Suzana Singano (Simba), Frank James Sekule (Simba), Frank Domayo Raymond (JKT Ruvu), Omega Sunday Seme (Yanga), Abdallah Kilala Hussein (Falcon, Pemba) na Ibrahim Rajab Juma (Villa Squad).
Hassan Saleh Dilunga (Ruvu Shooting), Alhaje Said Zege (JKT Ruvu), Jerome Lambele Reuben (Moro United), Atupele Green Jackson (Yanga), Simon Msuvan Happygod (Moro United) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo).
Mechi ya marudiano dhidi ya Sudan itachezwa jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.
Fainali za Afrika kwa vijana zitafanyika Machi mwakani nchini Algeria. Timu nne za juu kwenye fainali hizo zitacheza Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi Julai mwaka huu.

Comments