NGORONGORO HEROES YAIBAMIZA SUDAN 3-1


TIMU ya soka ya taifa ya vijana wenye umri  chini ya miaka 20 ' Ngorongoro Heroes' imeanza leo vema  mechi yake ya kwanza ya raundi ya awali kuwania kufuzu fainali za Afrika vijana wa umri huo, baada ya kuwafunga wenzao wa Sudan kwa mabao 3-1.
Mshambuliaji wa timu hiyo anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Tp Mazembe ya Jamhuri yua Kidemokrasia ya Congo (DRC) Thomas Ulimwengu aliifungia Ngorongoro Heroes bao la kwanza,  kabla ya Ramadhani Singano kufunga la pili dakika  na la tatu likipachikwa na Simon Msuva.


Comments