NGORONGORO HEROES WAZUIWA TAIFA


KATIKA hali ya kushangaza, timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, juzi ilizuiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Katika kile kilichoonekana ni mipango mibovu ya watendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), timu hiyo ilifika uwanjani hapo ikiwa na Kocha wake, Mdenish, Kim Poulsen, lakini katika mazingira ya kutatanisha, walinzi wa uwanja huo waligoma kufungua milango ili gari la timu hiyo liingie.
Kutokana na hali hiyo, Kocha Poulsen, alionekana akiwasiliana na viongozi wa TFF, lakini mara ghafla alikata simu na kuamuru msafara wa timu yake ugeuze na kuondoka eneo hilo.
Alipoulizwa kiongozi mmojawapo wa TFF kuhusiana na tukio hilo, alielezea kushangazwa na hatua hiyo na kubainisha kuwa timu hiyo ni ya taifa hivyo haikupaswa kuzuiliwa kuingia kufanya mazoezi.

Comments