MAN U KATIKA MAJONZI TELE


KLABU ya Manchester United iko katika majonzi kufuatia kifo cha Mkurugenzi wake wa zamani,  Amer Midani.
Mzaliwa huyo wa Beirut mwaka 1957, Mr Midani alijiunga na klabu hiyo ya Old Trafford mwaka 1987 wakati United ilipoinunua klabu ya mpira wa kikapu ya Manchester Giants, ambayo alikuwa Mwenyekiti wake.
Awali alikuwa raia wa Lebanon na bingwa wa michuano ya watoto ya table tennis akiwa ana umri wa miaka 15 na alihamia England akiwa ana umri wa miaka 18.

Comments