MAMA MZAZI WA MAREHEMU KANUMBA KUAMUA MWANAKE AZIKWE WAPI

WAKATI Polisi inaendelea na uchunguzi, ratiba ya mazishi ya aliyekuwa nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba imetolewa.
Nyota huyo wa filamu ya The Shock ataagwa Jumanne kuanzia saa 4:00 kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar es Salaamna kufuatiwa na mazishi yake.Kamati ya Mazishi iliyoundwa haraka inaundwa na Wajumbe, Eric Shigongo, Mtitu Game, Asha Baraka, Issa Muusa ‘Cloud’, Dilesh Solanki, Ruge Mutahaba na William Mtitu.abari zilizopatikana msibani hapo, Sinza, Dar es Salaam zinasema kwamba Kamati inasumburi mama wa marehemu, ili waamue azikwe wapi.Mama wa Kanumba anatokea Bukoba na leo anatarajiwa kulala Mwanza kabla ya kupanda ndege kesho asubuhi kuja Dar es Salaam.Kamati inataka mamahuyo afike Dar es Salaam, imshawishi azikwe Dar es Salaam.Siku za mwishoni za uhai wake, Kanumba aliingia katika mgogoro na baba yake na hadi sasa haijulikani kama atashiriki mazishi hayo.Kanumba alifariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo na chanzo cha kifo chake inaelezwa ni kugombana na mpenzi wake, mwigizaji mwenzake, Lulu.

Comments