MAJERUHI SI KITU KWANGU-DIABY


KIUNGO Abou Diaby (pichani kulia) amesema matatizo ya majeruhi si kitu akilinganisha na matatizo ambayo wachezaji wengine wamepitia.

Bunduki ya zamani Arsenal, Fabrice Muamba bado anaendelea na tiba baada ya kupata matatizo ya moyo uwanjani akiichezea Bolton mwezi uliopita, wakati beki wa kimataifa wa Ufaransa, Eric Abidal anatakiwa kwenda kufanyiwa operesheni ya ini.

Diaby amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara ambayo yamemfanya acheze mechi tatu msimu huu, lakini hana wasiwasi na anaamini mambo yatakuwa sawa.

“Kusema ukweli kuna mazingira fulani ambayo unayafikiria juu ya mustakabali wako, lakini ni muhimu kukubaliana nayo,” alisema.

“Wakati maumivu yanatokea, yanakuingia na huwezi kupata ishu, ni vigumu sana. Kitu pekee unachoweza kufanya ni kuangalia mbele na kukubali.

“Kuna hali mbaya zaidi katika maisha kuliko inayonikabliT mimi, hata kwenye soka, ukiangalia kilichowatokea Muamba au Abidal. Mimi, si kitu.”








Comments