MADONNA AVUNJA REKODI YA ELVIS


Madonna

MADONNA amevunja rekodi ya Elvis na kuwa mwanamuziki wa kujitegemea mwenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya Uingereza – lakini huwezi amini wanawe hawapendi nyimbo zake.
Malkia huyo wa Pop alivunja rekodi ya Mfalme huyo jana, wakati albamu yake ya sasa, MDNA, iliposhika namba moja katika chati za UK —  hiyo ikiwa mara ya 12 kushika namba katika historia yake, wakati Elvis aliweza mara 11.
Hayo ni mafanikio makubwa kwa Madge wakati wimbo uliopita, Give Me All Your Luvin', ulishika nafasi ya 37 tu kwenye chati hizo Februari.
Watu wanamzimikia kinoma Madonna, tena kwa miaka kibao, lakini watoto wake — Lourdes, Rocco, Mercy na David — wako tofauti kabisa.
Madonna alisema: "Watoto wangu wako wawazi sana hasa inapokuja juu ya kitu ambacho hawakipendi. Hawapindipindi daima. Wanasema tu, 'Mum, toa huo wimbo hata kama ni wa kwangu. Inauma, lakini angalau ni wawazi."

Comments