MACHEDA AMSONONESHA FERGUSON


KOCHA Sir Alex Ferguson amemtetea Federico Macheda kwamba ataibuka tena katika kipindi cha kucheza kwake kwa mkopo na kurejea kufanya vitu Manchester United.
Mshambuliaji huyo Italia hakuwa na furaha akiichezea Sampdoria msimu uliopita na alipotua QPR, baada ya kuondoka kwa kocha Neil Warnock na Mark Hughes kuchukua nafasi, alisajili wachezaji wenye majina makubwa kama Djibril Cisse na Bobby Zamora Januari.
Hiyo ilitokana na matatizo ya kifundo cha mguu yaliyomuandama Macheda na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza Loftus Road hadi akarejea Manchester wiki iliyopita kwa matibabu.
Bado kocha Ferguson ana matumaini na kijana huyo mwenye umri wa miaka 20 na anaamini jinamizi la majeruhi linalomuandama hivi sasa litafika mwisho na ataanza kung’ara tena.

Comments