LULU APANDISHWA MAHAKAMA YA KISUTU LEO AKIKABILIWA NA KESI YA KUMUUA KANUMBA


MSANII wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kama 'Lulu' leo   asubuhi amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kusomewa mashtaka yake kufuatia kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Charles Kanumba. 
Lulu amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Kanumba yaliyotokea huko sinza Vatcan jijini Dar es Salaam aprili 7 mwaka huu. 
Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwani  mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ambapo kesi hiyo  imeahirishwa tena na itaanza kusikilizwa tena aprili 23 mwaka huu.
 Awali nyota huyo alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali na kwa kasi ya ajabu hali iliyopelekea waandishi wa habari kutopata wasaa hata wa kupiga picha, kabla ya kuondolewa mahakamani hapo kwa gari aina ya Suzuki Grand Vitara yenye usajili namba T848 BNV na nambari za kwenye kioo PT 2565.

Comments

  1. du, sidhani kama huyu mtoto ataepukana na 'hiki kikombe', ila itategemea na ripoti ya daktari...

    ReplyDelete
  2. kila siku usie sikiliza lamkuu huvunjikaa Guu.

    ReplyDelete

Post a Comment