KUZIONA NGORONGORO NA SUDAN BUKU TATU


Thomas Ulimwengu anayetarajiwa kuibebaa Ngorongoro keshokutwa

KIINGILIO cha chini cha mechi ya kuwania kucheza Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan itakayochezwa Jumamosi (Aprili 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 3,000.
 Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo amesema kwamba mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni, na viingilio vingine vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati VIP itakuwa ni sh. 15,000.
Alisema Sudan inatarajia kuwasili leo mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines ikiwa na msafara wa watu 30 na itafikia hoteli ya Rungwe iliyoko maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam. Jioni itafanya mazoezi Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Ngorongoro Heroes tayari iko kambini chini ya Kocha Kim Poulsen, na leo inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Sudan yenyewe itafanya mazoezi kwenye uwanja huo kesho.
Alisema kesho (Aprili 20 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutakuwa na mkutano kati ya makocha wa timu zote mbili na Waandishi wa Habari.

Comments