KIKWETE AWAPA POLE YANGA


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAMBIRAMBI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti  wa klabu ya mpira wa miguu ya Young Africans Sports Club (Yanga)  Bw. Lyod Nchunga kufuatia kifo cha Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, wakili Theonist Rutashoborwa, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo kutokana na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.
“Nimepokea kwa Masikitiko na huzuni sana taarifa za wakili Theonist Rutashoborwa kilichotokea usiku wa Kuamkia leo, hili ni pigo na pengo kubwa katika klabu ya Yanga katika kipindi hiki cha kushiriki ligi kuu” Rais amesema.
“Naomba unifikishie rambirambi zangu za dhati kwa familia, wachezaji na wana Yanga wote kwa kuondokewa na Mjumbe wao katika kipindi hiki” Rais ameongeza na kuwataka wana Yanga wawe wavumilivu wakati wa msiba huu na kumuombea Bw. Rutashoborwa mapumziko mema ya Milele.
……………Mwisho…………

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu-Dar-Es-Salaam
12 April, 2012

Comments