KANUMBA KUAGWA J'4 VIWANJA VYA LEADERS, KUZIKWA SIKU HIYOHIYO


MMOJA ya waombolezaji WEma Sepetu na rafiki zake wakiwasili kwenye msiba wa msanii wa filamu nchini Steven Kanumba eneo la Sinza, Vatican jijini Dar es Salaam.Kanumba ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo anatarajiwa kuzikwa jumanne ambapo kabla ya maziko hayo ataagwa kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waombolezaji waliojitokeza kwenye msiba wa Kanumba na hapo wengi wao ni waigazaji wa filamu za bongo


Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo naye ni mmoja ya waombolezaji waliojitokeza katika msiba huo

Vilio vilitawala,wengine walizimia yaani ni simanzi kwa kweli
Cheni akibadilishana mawazo na waombolezaji waliojitokeza

mmoja ya waigizaji wa bongo muvi Irene Poul akilia kwa uchungu katiia msiba huo, msanii huyu ni mmoja ya waigizaji walioibuliwa na marehemu na tayari ameshajipatia umaarufu kupitia kazi zake kadhaa.

Comments