JUMA KASEJA AMKUMBUKA KANUMBA

 TANZANIA One Juma K Juma amemkumbuka nguli wa tasnia ya filamu nchini Steven Kanumba ambaye alifariki usiku wa kuamkia Aprili 7 nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam.
Kaseja anayeidakia timu ya soka ya Simba alitinga katika dimba la Taifa jana wakati timu yake ilipokwaana na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.
Kaseja aliingia uwanjani nakiwa ametinga tishet nyeupe iliyoandikwa 'RESPECT U ROREVER KANUMBA' hali inayoonyesha ni jinsi gani ameguswa na msiba wa msanii huyo ambaye kifo chake kimeaacha simbanzi kwa watu wengi.

Comments