JESHI LA SIMBA LATUA FRESH ALGERIA TAYARI KWA MAANGAMIZI

Simba ndani ya Algeria
KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imefika salana Algeria jioni hii na kuelekea katika mji wa Setif tayari kwa mechi dhidi ya wenyeji ES Setif, Ijumaa.
Simba ikiwa na hazina ya mabao 2-0 itaingia kwenye mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili Kombe la Shirikisho ikihitaji sare ya ugenini au kufungwa si zaidi ya 1-0 isonge mbele.    
Simba iliyoondoka Dar es Salaam Alfajiri ya Jumatatu, ililala Cairo Misri kabla ya kuelekea Algeria.

Comments