JESHI LA POLISI LAMTIMUA KAZI ASKARI ALIYEKUTWA NA MISOKOTO YA BANGI DISKO

Na Rodrick Mushi,Moshi.
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limemfukuza kazi askari wake aliyefanya vurugu disko pamoja na kukutwa na misokoto minne ya bangi.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Absalom Mwakyoma  alisema kuwa jeshi hilo limemfukuza rasmi askari huyo baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na makosa mawili ya jinai.
Tukio la  askari aliyefukuzwa kuingua kwenye ukumbi wa starehe na kufanya vurugu lilitokea april 2 mwaka huu baada ya askari huyo  ambaye aliingia eneo hilo majira ya saa 6 usiku na kuanza kufanya vurugu pamoja na shambulio kwa mmliki wa Christopher Shayo pamoja na mlinzi.. 
Mwakyoma alisema kuwa askari huyo mwenye namba G8415 Deogratiasi  Matious (22) alifanya fujo na kasha kumshambulia mlizi wa ukumbi wa disko wa Pub Alberto   Rajabu Mohamedi na kummuumiza kwa kumngata kwenye mkono.
Hata hivyo alisema kuwa kosa lingine alilofanya askari huyo aliyefukuzwa ni pamoja na kukutwa na misokoto 4 ya bangi ikiwa mfukoni mwake,hivyo makosa hayo mawili ndio yaliyomfukuzisha kazi.
Alisema kuwa jeshi hilo limefanya hivyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko kwa baadhi ya askari kukiuka maadili ya jeshi hilo.
Katika wakati mwingine alisema kuwa baada ya kufukuzwa kazi atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili,na kazi hiyo imekabidhiwa kwa mwanasheria wa Serikali ili kulifikisha shauri hilo Mahakamani.
Mwakyoma alisema kuwa kwa mwaka 2011/2012 askari wapatao 18 wameshafukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kukiuka maaadili ya Jeshi hilo.





Comments