HISPANIA INATISHA, YAINGIZA TATU NUSU FAINALI EUROPA LEAGUE


Beki wa Atletico Madrid, Diego Godin akishangilia baada ya kutinga Nusu Fainali

KLABU za Hispania zimeng’ara katika usiku huu katika michuano ya Ulaya,  baada ya Athletic Bilbao, Atletico Madrid na Valencia kutinga Nusu Fainali ya Europa League sambamba na Sporting Lisbon ya Ureno.
Bilbao imetoka sare ya 2-2 na Schalke na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa wa 6-4 aggregate, Valencia imeikung’uta AZ Alkmaar 4-0 na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-2, na Atletico imeshinda 2-1 dhidi ya Hannover na kupigta kwa jumla ya wa 4-2.
Sporting imetoa sare ya 1-1 na Metalist Kharkiv na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2.
Sasa, Sporting itacheza na Bilbao na Atletico itawakabili Valencia. Klabu za Hispania pia zilifika hatua hiyo mwaka 2007.
Mapema wiki hii, Barcelona na Real Madrid zilitinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa, zikungana na Bayern Munich itakayocheza na Real na Chelsea itakayocheza na Barca.

Comments