HASIRA ZETU KWA MAN CITY- VAN PERSIE


Van Persie na Theo

MSHAMBULIAJI Robin van Persie amejisikia vibaya baada ya kipigo cha Jumamosi kutoka kwa Queens Park Rangers, lakini amesema makali ya Arsenal yatarejea watakapokwenda kucheza na Manchester City.
Mholanzi huyo alishuhudia rekodi ya timu yake kushinda mechi saba mfululizo ikizimwa kwenye Uwanja wa Loftus Road, shukrani kwao Adel Taarabt na Samba Diakite kwa mabao yao siku hiyo.
Arsenal inabaki nafasi ya tatu, lakini inalingana kwa pointi na Tottenham, ambayo iliifunga Swansea City 3-1 jana.
"Kila mmoja amesikitishwa, lakini kuelekea mwishoni mwa wiki nina uhakika kwamba makali yatakuw akama yalivyokuwa," alisema Van Persie. "Tutakuwa na siku kadhaa za masikitiko, lakini baada ya hapo, fikra zetu ni kwa Manchester City.

Comments

  1. Dada wewe ni mwandishi wa habari, unapochukua habari hii bila kuquote umeiota wapi ni kosa...walau tupeni na sisi heshima...

    ReplyDelete

Post a Comment