HABARI NZURI KWA MASHABIKI WA SIMBA SC

HABARI nzuri ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa klabu ya Simba Mzambia Felix Mumba Sunzu (pichani)ambaye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya Tumbo amepona na huenda akawemo kwenye kikosi cha timu hiyo kitakacokwaana na Moro United jumatatu katika mchezo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga ameiambia mamapipiro blog kwamba kupangwa ama kutopanghwa kwa mchezaji huyo kunategemeana na uamuzi wa kocha lakini yupo fiti kabisa.
Alisema kikosi cha timu hiyo kilichopewa mapumziko ya siku moja kinaingia kambini jioni ya leo kwenye hoteli ya Beach iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Alisema kupona kwa Sunzu kunafanya kikosi chgote cha timu hiyo kuwa imara hivyo kufanya maandalizi yake ya mechi za ligi kuu na mchezo wao wa kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) kwenda kama ilivyopangwa.

Comments