GUNNERS KUIPALILIA UBINGWA MAN UNITED UNITED LEO?


Van Persie
INGAWA Sergio Aguero alikuwa anaumwa kifundo cha mguu, lakini inaaminika atakuwa fiti kumbeba kocha wake Roberto Mancini leo dhidi ya Arsenal.
Joleon Lescott amepona maumivu ya nyonga lakini inaweza kuwa ajabu kumuona kwenye kikosi cha Manchester City katika mchezo huo muhimu.
Micah Richards anaumwa kichwa alilazimika kuiacha mechi kati ya sare ya 3-3 kati ya City na Sunderland ikiendelea mwishoni mwa wiki iliyopita na nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Pablo Zabaleta katika beki ya kulia.
Samir Nasri ambaye naye yuko fiti anawania nafasi kwenye kikosi cha kwanza kucheza dhidi ya timu yake ya zamani, baada ya kukosa mechi iliyopita.
Arsenal ina kikosi kamili na ni kocha tu yeye mwenyewe kuchagua amtumie nani katika vita la leo.
Jack Wilshere anayeumwa kifundo cha mguu ataendelea kuwa nje ya Uwanja, kama ilivyo kwa viungo wenzake, Emmanuel Frimpong (goti), Abou Diaby (nyama) na Francis Coquelin (nyama). Beki Per Mertesacker anayeumwa kifundo cha mguu pia hatacheza kwenye Uwanja wa Emirates Leo..

JE WAJUA?
•Arsenal ilishinda mechi sita mfululizo kabla ya kusimamishwa na QPR kwa kichapo cha 2-1 mwishoni mwa wiki iliyopita, na miongoni mwa mechi ilizoshinda ni dhidi ya Tottenham, Liverpool na AC Milan.
•Manchester City imekuwa butu ugenini kwa miezi kadhaa sasa.
•Mechi zote baina ya timu hizo zinazowania kucheza Ligi ya Mabingwa msimu huu ziliisha kwa Mancini kushinda 1-0.
•City wamefungwa mechi zote nne msimu huu ambazo Mario Balotelli na Edin Dzeko wamecheza pamoja kikosini.
•Pamoja na kwamba City iliifunga The Gunners katika Kombe la Ligi Uwanja wa Emirates, Novemba, mara ya mwisho timu hiyo kuifunga Arsenal katika Ligi Kuu ilikuwa Oktoba. 4, 1975.
 •Balotelli amefunga mabao kila baada ya dakika 94 msimu huu, ambayo ni kiwango kizuri katika Ligi Kuu kwa wachezaji wote ambao wamecheza kiasi cha dakika 1000.
•Theo Walcott anafagiliwa na mashabiki wa Arsenal, lakini winga huyo amefunga au kutoa pasi za mabao 15 katika mashindano makubwa tangu msimu wa 2011-12 uanze. Wayne Rooney ni Muingereza pekee mwenye rekodi nzuri.
•Iwapo Manchester City itashinda itapunguza pengo la pointi inazozidiwa Manchester United. Lakini pia pengo hilo litategemea na matokeo ya Manchester United na QPR, ambayo itachezwa kabla ya mehi ya Arsenal Vs City. Kwa sasa City inazidiwa pointi tano.
•Aleksandar Kolarov amepiga krosi 16 katika nafasi za wazi mwishoni mwa wiki iliyopita ambayo ni idadi kubwa msimu huu. Winga wa Wolves, Matt Jarvis alipiga 17 dhidi ya Newcastle Oktoba, mwaka jana.

VIKOSI VYA LEO:
ARSENAL: Szczesny, Sagna, Koscielny, Vermaelen, Gibbs, Arteta, Song, Rosicky, Walcott, Van Persie na Gervinho.
MANCHESTER CITY: Hart, Zabaleta, K Toure, Kompany, Kolarov, Barry, Y Toure, Nasri, Aguero, Balotelli na Dzeko.

Comments