GIGGS AONYA KUHUSU QPR

Giggs
MKONGWE wa  Manchester United, Ryan Giggs amesema kwamba mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, Mark Hughes atawapa mtihani mgumu mwishoni mwa wiki.
Queens Park Rangers itakuwa mgeni wa United kwenye Uwanja Old Trafford.
Wakati ikimenyana na United ugenini, Giggs anahofia uzoefu wa baadhi ya wachezaji wapya wa QPR utawapa wakati mgumu.
"Mark ameongoza klabu kadhaa chache, sasa si kocha mpya tena. Atawaongoza na kuwaandaa vizuri kama tu timu nyingine zinazokuja Old Trafford. Watafanya iwe mechi ngumu kwetu," Giggs aliiambia ManUtd.com.
QPR ni timu ya tatu iliyo hatarini kushuka daraja kukutana naUnited katika mechi zake nne zilizopita, baada ya Mashetani hao Wekundu kuzifunga Wolves na Blackburn Rovers.

Comments