GANGWE MOBB KUWASINDIKIZA CHEKA, MAUGO KESHO


WAKATI pambano la kuwania bingwa wa ngumi unaotambuliwa na IBF Africa kati ya Mada Maugo na Francis Cheka ukitarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba, mabondia hao kila mmoja ametamba kumtwanga mwenzake.
Mabondia hao watapambana katika uzito wa Kati, katika pambano la raundi 12 ambapo pamoja na ubingwa mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Mark 11 Grande lenye thamani ya shilingi milioni 8.
Wakizungumza na mamapipiro blog wakati wa kupima uzito leo, mabondia hao kila mmoja alitamba kumtwanga mwenzake kwa Ko.
Kwa upande wake Maugo alisema kuwa kwa maandalizi aliyoyafanya ana uhakika wa kushinda mpambano huo, lakini akiwaomba waamuzi wafanye haki katika maamuzi yao ili mshindi apatikane kihalali.
“muda wa kuongea umekwisha hivyo vimebaki vitendo, nipo tayari kwa mpambano huo lakini kubwa ni kuwaomba waamuzi kutenda haki na mshindi apatikane kihalali,”Alisema.
naye Cheka alisema Maugo si lolote kwake na atamfundisha kazi mapema tu na amejiandaa ipasavyo na mpambano huo ambao anaamini ataibuka na ushindi.
Naye mwandaaji wa pambano hilo Lucas Ruta kupitia kampuni ya Kitwe General Traders, alisema kwamba maandalizi yamekamilika ambapo kutakuwa na ulinzi wa uhakika kwa mali na mashabiki watakaojitokeza kushuhudia.
Alisema pambano hilo litatanguliwa na mengine nane ya utangulizi hivyo amewaomba mashabiki wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi ambapo kundi la Gangwe Mob litatoa burudani.

Comments