FLORA MVUNGI AFUATA NYAYO ZA SHILOLE


MSANII nyota katika Bongo Muvi Flora mvungi ameonekana kufuata nyayo za msanii mwezake Shilole baada ya naye kuamua ikujitosa katika fanmi ya muziki.
Flora ameiambia mamapipiro blog kwamba kujitosa huko katika muziki ni sehemu nyingine ya kuonyesha kipaji chake kingine alichojaliwa na mwenyezi mungu.
Alisema kwa kudhihirisha kuwa amedhamiria mesharekodi singo yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la 'Sinaga'
Alisema pamoja na kugeukia muziki bado ataendelea na kazi yake ya uigizaji wa filamu za kibongo.
Flora ambaye aliibukia katika fani ya urembo na kutwaa taji la Miss Pwani, Kanda ya Mashariki hadi kutinga fainali za Miss Tanzania mwaka 2009.

Comments