RAGE ANCHARUKA UJIO WA TP MAZEMBE

SIKU chache baada ya kuwepo kwa utata juu ya ujio wa klabu yaTp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki na klabu ya Simba, uongozi wa Simba umewatoa hofu mashabiki wa Simba na wa soka kwa ujumla juu ya ujio huo.
Hivi karibuni aliyewahi kuwa mdhamini wa Simba na Makamu Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo Azim Dewji alitangaza kuileta Tp Mazembe kwa ajili ya kuipa makali Simba ambayo inatarajiwa kucheza mechi ya kombe la Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage ameiambia mamapipiro blog kuwa  yeyue na makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Azim Dewji wamekuwa wakifanya mawasiliano ya mara kwa mara na mmliki wa TP Mazembe Mose Katumbi.
Alisema anashangazwa na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari zikimnukuu kocha msaidizi wa Tp Mazembe Lamine Ndiaye  kutokuwa na taarifa za ziara hiyo kitu ambacho hakina mantiki yoyote kwa kuwa kocha kazi yake ni kufundisha tu.
“Kama mtu anataka uhakika awasiliane na Katumbi ama katibu wake Kitenge, sisi tunafanya mazungumzo wenyewe kwa wenyewe (viongozi) na mambo yakiwa tayari wanapewa taarifa wengine ndiyo maana hata baadhi ya viongozi wenzangu wea Simba hawana taarifa rasmi,”Alisema Rage.
Rage aliongeza kuwa mipango kuhusiana na ujio wa timu hiyo ambayo nayo inatarajiwa kukwaana na El Mereikh ya Sudan katika Ligi Ya mabingwa barani Afrika yanakwenda vema na kama kutakuwa na mabadiliko yoyote watatoa taarifa rasmi.Katika hatua nyingine, Rage amempongeza Dewji kwa kutimiza ahadi yake ya kuwakabidhi wachezaji wa timu hiyo kitita cha shilingi milioni 15 baada ya kuitoa Es Setif ya Algeria na kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF).

Comments