DIAMOND AMCHANA BOB JUNIOR


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amemponda bila ya kumtaja jina aliyekuwa mtayarishaji wake, Bob Junior kwa kitendo chake cha kukataa kumpatia lebo msanii Ommy Dimpoz.
Akielezea mkasa huo wakati alipomsindikiza msanii Ommy kupokea tuzo yake ya Kili music ndipo alisema “Mara ya kwanza nilipompeleka mshikaji wangu Ommy kwa mtayarishaji wangu wa zamani na kumuomba afanye naye kazi, alinisikitisha pale alipokataa na kusema hawezi kuimba, lakini cha kushangaza leo anachukua tuzo na huyo mtayarishaji hajachukua hata moja.”
Mtayarishaji aliyewahi kuwa lebo na Diamond alikuwa Bob Junior na ndiye pia hajawahi kuchukua tuzo za kili.

Comments

  1. kwa kupiga sufi aka pamba unajitahidi bana big up tandale boys

    ReplyDelete
  2. kuchukua tuzo sio kitu bhana kuna the best lakini basi tu

    ReplyDelete
  3. Wewe kuchukua tuzo unajiona umefika@Diamond?

    ReplyDelete
  4. Watanzania acheni unafki kwani 2zo na izo pamba c ni zakwake acheni m2 avae anapota eeh na akikosa je mnaanza kumcheka kwamba amefuli,muacheni ni wakat wake sasa kutanua,Au ulitaka upwe wewe nini izo 2zo?

    ReplyDelete

Post a Comment