DHL WAJIVUNIA UJIO WA KOMBE LA UEFA


KAMPUNI ya Usafirishaji wa Vifurushi ya DHL, imesema ujio wa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu England linaloshikiliwa na Mashetani Wekundu, Manchester United ya Uingereza jijini Dar es Salaam hivi karibuni umeleta faraja kwao na Watanzania kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Maneja wa Kampuni hiyo nchini, Blaise De Souza, alisema, ziara hiyo imetoa fursa kwa Wananchi na wapenda soka kulishuhudia.
“Kuja kwa kombe hilo, kumetoa fursa kwetu na imeonyesha kwa jinsi gani tunafanya kazi kubwa kwa wateja wetu,” alisema.
Alisema, pia imetuo fursa kwa wafanyakazi wao kukutana ana kwa ana na baadhi ya nyota wa zamani wa Man U, wakiwemo Quinton Fortune na Gary Bauley.
Aidha alisema, DHL imefanya kazi kubwa kulileta kombe hilo na kutoa fursa kwa Watanzania kulioana na kupiga picha nalo.

Comments