COASTAL UNION WAOMBA KUWE NA 'KANUMBA DAY'

WAKATI Taifa likiendelea kuomboleza kifo cha nguli wa filamu nchini Steven Charles Kanumba, klabu ya soka ya Coastal Union ya Tanga imeomba kuwepo na siku maalum kwa ajili ya kumkumbuka msanii huyo 'Kanumba Day'.
Kanumba ambaye alizikwa jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya kufariki usiku wa kuamkia Aprili 7 nyumbani kwake Vatican City, Sinza baada ya ubongo wake kushindwa kufanya kazi .
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya klabu hiyo Salim Bawazir amesema kifo cha msanii huyo ni pigo kwa taifa na wadau wa tasnia ya filamu barani Afrika na dunia kwa ujumla.
Alisema kutokana na mchango mkubwa alioutoa msanii huyo katika kuendeleza medani ya filamu nchini ni vema kama angekuwa akienziwa kila mwaka.
"Kanumba ameacha pengo ambalo kuzibika kwake itachukua muda mrefu, hivyo ingekuwa ni busara kuenziwa kwa kuwepo na siku yake maalum,"Alisema.

Comments