COASTAL UNION WAING'ONGA YANGA

KLABU ya soka ya Coastal Union ya Tanga imesema kuwa kupokwa pointi kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu Bara, Yanga ni fundisho kwa klabu nyingine hapa nchini ambazo hazifuati sheria 17 za mchezo.
Hatua hiyo inafuatia kamati ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuipoka Yanga pointi tatu na mabao matatu na kuzipeleka Coastal baada ya kumchezesha beki wake Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alikuwa anatumikia adhabu ya kadi.
Kocha msaidizi wa Coastal Union amesema wamepokea kwa shangwe hatua hiyo kwani inazidi kuwapandisha katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inaelekea ukingoni.

Comments