CHOKI:NACHUKIWA KWA KUHAMISHA WANAMUZIKI


MWIMBAJI na Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki alisema kwamba kwa sasa amejikuta akichukiwa na Mkurugenzi wa African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka kwa madai ya kuhamisha wanamuziki wake na kuwaajiri.
Choki aliyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na televisheni moja maarufu ya jijini hapa ambako alisema anashangaa kumuona mkurugenzi wake wa zamani Asha Baraka  akimchukia wakati anajua waimbaji wanahama kwa ajili ya kutafuta maslahi.
“Kuhama kwa waimbaji ni kujitafutia maslahi lakini nashangaa kwa nini Mkurugenzi mwenzangu wa Tweanga anachukia hilo. Si kwangu bali kwa bendi nyingi tu,” alisema.

Comments