CHELSEA NA BARCA, REAL NA BAYERN NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

Meireles
KLABU ya Chelsea usiku huu imeifunga Benfica ya Ureno mabao 2-1, wafungaji Frank Lampard na Raul Meireles na kufuzu kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1.
Kwa ushindi huo kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, Chelsea ya England sasa itakutana na mabingwa watetezi, Barcelona ya Hispania kwenye Nusu Fainali.
Katika mchezo mwingine, Real Madrid ya Hispania imeshinda mabao 5-2 dhidi ya APOEL Nicosia ya Cyprus, Cristiano Ronaldo akifunga mabao mawili na kutimiza mabao 49 msimu huu.
Real sasa imetinga Nusu Fainali kwa ushindi wa jumla wa 8-2 na itakutana na Bayern Munich ya Ujerumani katika Nusu Fainali.

Comments