BENITEZ ASEMA BARCA HII HAIFIKII AC MILAN YA ARRIGO SACCHI KWA UBORA


Benitez

KOCHA wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez anafikiri kwamba Barcelona siyo timu bora daima kama anavyoamini kwamba AC Milan ya Arrigo Sacchi ilikuwa bora kuliko kikosi cha sasa cha wana Catalan.
Barcelona ambayo imetwaa mataji mawili mfululizo ya Ligi ya Mabingwa katika misimu mitatu iliyopita na kwa mara nyingine tena inapewa kubwa ya kutwaa tena taji hilo.
Pamoja na hayo, kwa maoni yake Benitez ni kwamba Milan ya mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 kilikuwa ‘levo’ nyingine kabisa.
" Barcelona ndio timu bora zaidi niliyowahi kuiona maishani mwangu? Kusema ukweli ni niliipenda sana AC Milan wakati wanacheza na akina [Marco] van Basten na [Ruud] Gullit na wachezaji wote [Arrigo] Sacchi akiwa kocha," alisema Benitez akihojiwa na fifa.com.
"Walikuwa wanafanya vizuri haswa, walitawala sana wakati huo. Barcelona wamekuwa zaidi au chini ya hapo, na unaweza kuona sasa Bayern Munich au wakati fulani [Manchester] United au Real Madrid wanaweza kushindana.
"Nakumbuka Real Madrid ilikuwa timu babu kubwa wakati huo na hawakuweza kufanya  kitu chochote dhidi ya Milan, hivyo ilikuwa tofauti kubwa. Lakini Barcelona ni timu kubwa kuiangalia."
Barcelona inamenyana na Milan katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Robo Fainali kwenye Uwanja wa Camp Nou kesho, baada ya mechi ya kwanza kumalizika kwa sare ya bila kufungana kwenye Uwanja wa San Siro wiki iliyopita.

Comments