MSONDO NGOMA WAANIKA RATIBA YAO YA PASAKA


BENDI kongwe ya muziki wa dansi Tanzania, Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ imetoa ratiba yao katika kusherekea Sikukuu ya Pasaka ambapo

wamesema kuwa wataanza kutoa burudani ndani ya Wipes Bar Mivinjeni
Kurasini, siku ya Ijumaa watakuwa Leanders Club Kinondoni, Jumamosi
watakuwa TCC Club Chang’ombe, Pasaka watakuwa Kata ya 14 Temeke na
Jumatatu ya Pasaka watakuwa sambamba na FM Academia ‘Wazee wangwasuma’.



Akingongea , Msemaji wa Msondo, Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa wameamua kutoa ratiba hiyo ili mashabiki wao waweze kujua nini
kinachoendelea ndani ya bendi yao.



Alisema kuwa hata hivyo tayari wamajipanga vizuri katika suala zima la kuwapa burudani mashabiki wao katika kusherekea sikukuu hii ya Pasaka.



“Msondo ipo kamili katika kutoa burudan na ndiyo maana imeamua kutoaratiba, hivyo tunaamini mashabiki wetu watakuja kwenye matamasha yetu
kwani bila wao sisi hatuwezi kusimama na kuimba,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa wanahitaji mashabiki wao kjitokeza kwa wingiili waone nini wanachowapa katika siku hizo zote kwani sikukuu ya
pasaka ni muhimu kusherekea na msondo ngoma bendi hiyo inayotamba na
vibao vyake vipya vya Suluhu wa Shabani Dede na Nadhiri ya Mapenzi wa
Juma Katundu pia watapiga nyimbo zao zote zilizotamba kipindi cha
nyuma alisema Super D

Comments