AZAM FC WALIA HUJUMA

WAKATI ligi kuu soka Tanzania bara ikiwa inaelekea ukiongoni, uongozi wa klabu ya Azam Fc umelia jkuwepo hujuma ya kutaka kuidhoofisha ili iweze kupotea katia harakati zake za kuwania ubingwa.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa taarifa za klabu ya Simba kumyakua nyota wake Mrisho Ngassa kwa ajili ya kuichezea timu hiyo katika msimu ujao na michuano ya kimataifa.
Ofisa habari msaidizi wa Azama Jaffer Idd aliimbia mamapipiro blog taaruifa hizo si za kweli na zina lengo la kuichanganya klabu hiyo katika kampeni yake ya kuwania ubingwa.
Alisema baadhi ya watu wasioitakia mema klabu hiyo wamekuwa wakizua mambo yasiyo ya msingi ili uongozi uache kuiangalia timu na kufuatilia taarifa zisizo na maana, hivyo amewataka mashabiki wa timu hiyo kuzipuuza.
Azam inayoshika nafasi ya pili katika ligi hiyo ikiwa na p[ointi 50 nyuma ya Simba yenye pointi 56 imebakiza michezo miwili kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.

Comments