AZAM FC MIKONONI MWA POLISI DOM


KIKOSI cha timu ya soka ya Azam Fc kimepiga kambi mjini  Dodoma tayari kwa pambano lao la ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya maafande wa Polisi Dodoma, itakayopigwa jumaosi katika dimba la Jamhuri mjini humo. 
Ofisa habari msaidizi wa Azam Fc Jaffer Iddy amesema kwamba kikosi chao kilichowasili mjini humo jana kipo katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo huo ambao wana uhakika watazoa pointi tatu.
Alisema pamoja na kujipanga vema kwa ushindi huo wanatarajia kupata upinzani mkali katika mchezo huo na hasa ikizingatiwa kuwa hatua hiyo ni lala salama hivyo kila timu inahitaji kushinda.
 Azam Fc inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikwa na pointi 47 huku Simba ikiongoza kwa pointi 50 na mabingwa watetezi wa ligi hiyo wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi  43 .

Comments