10 BORA WA NGUMI KUSAKWA MEI 4



MASHINDANO ya kumi bora ya mchezo wa masumbwi yanatarajia kufanyika mei 4 katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es Salaam. 
Akizungumza na waandishi wa habari Kocha wa kimataifa wa mchezo wa Ngumi RajabuMhamila 'Super D' alisema vijana wengi wamejitokeza kushiriki michuano hiyo yenye lengo la kupanga viwango vya mabondia. 
Aliwataja baadhi ya mabondia watakaopambana siku hiyo ni Ibrahim Class atakaezichapa na Idi Mnyeke, Amiri Macho atazidunda na West Scorpion,Charo Issa na Hamis Nassoro,Athumani Sadara na Abuu Mtambwe, Hassan Mijugu ataoneshana kazi na Saidi Ally, Sandari Nyambara na Pascal Ignus. 
Pamoja na mapambano mengine yatakayokuwa katika uzito tofauti tofauti vijana wengi wamejitokeza hivyo tunaomba sapoti ya aina yoyote kutoka kwa wadau wa mchezo wa masumbwi kufanikisha mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kinyogoli Fondition kwa ajili ya kuwapanga katika viwango mbalimbali vya ubora wa wachezaji. 
Alitaja baadhi ya maitaji kwa siku hiyo ni kuwa maji kwa wachezaji wakati wakiwa ulingoni,zawadi za kuwatia moyo wachezaji pamoja na madawa mbalimbali yatakayotumika kwa ajili ya kuwapatia mabondia huduma ya kwanza alisema Super D. 
Kwa yoyote mwenye nia ya kusaidi mashindano hayo kwa namna moja au nyingine anaweza kuwasiliana
na kocha Mkongwe Habibu Kinyogoli kwa namba ya simu 0655928298 au unaweza fika katika klabu ya Amana CCM iliyopo Ilala Dar es Salaam vilevile waweza kuwasiliana
na kocha Super D

Comments