YANGA SC YAWAPIGA DONGO COASTAL UNION

YANGA imesema kwamba wachezaji wote wapo fiti na wenye viwango vya hali ya juu hali inayowapa utayari wa kucheza mechi yoyote bila hofu.
Yanga imetoa kauli hiyo kufuatia  viongozi wa Coastal Union kuanza kulala kwa nyakati tofauti baada ya kuona nyota wa Yanga waliofungiwa wamesitishiwa adhabu zao kwa muda.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba kelele za Coastal haziwanyimi usingizi kwani hata kama wachezaji wao watarejeshwa kifungoni wanao wachezaji ambao wanaweza kuitumikia vema klabu yao.
"Ndiyo maana kuna wachezaji wengi tunaosajili, sisi tunajiamini kuwa tunakikosi kizuri ambacho kinaweza kukabiliana na timu yoyote, nawashangaa hao Coastal wanavyotapata tangu wachezaji wetu waondolewe kifungo kwa muda,"Alisema Sendeu.
Yanga na Coastal zinatarajiwa kumenyana mwishoni mwa wiki hii mjini Tanga katika mechi ya ligi kuu bara.
Mwishoni mwa wiki iliyopita mwenyekiti wa kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Kamishna Mstaafu wa Polisi Alfred Tibaigana aliwafungulia baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao walifungiwa kwa nyakati tofauti na kamati ya Ligi baada ya kumpiga mwamuzi Israel Nkongo wakati timu hiyo ilipokwaana na Azam Fc katik uwanja wqa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Comments