YANGA SC WAENDELEA KUTALII DAR

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara wameendelea na mpango wao wa kufanya mazoezi kwenye viwanja tofauti ambao hii leo wameibukia katika Uwanja wa Tipper uliopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Yanga ambayo inajinoa kwa ajili ya michezo yake iliyosalia kwenye ligi hiyo wiki hii imekuwa ikifanya mazoezi kwenye viwanja tofauti ambapo tayari imeshafanya hivyo kwenye viwanja vya sekondari ya Loyola, Shule ya Kimataifa (IST) na uwanja wao wa Kaunda.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema kuwa lengo la kuhamahama huko ni mapendekezo ya kocha wao mkuu Kostadin Papic.
Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 43 itaendelea na harakati zake za kutetea ubingwa machi 31 itakapokwaana na Coastal Union ya Tanga.



Comments