YANGA KUONDOKA NA POINTI TATU LEO?


MABINGWA watetezi  wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga leo watakuwa na kazi moja tu ya kusaka pointi tatu kupitia mchezo wao na Villa Squad utakaopigwa katika Uwanja wa Taifa, imefahamika.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu alisema kikosi chake kipo katika hali nzurti na wamejipanga vema kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ili kujiweka katiika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.
“Unajua sasa hivi ni kipindi chja lala salama hivyo ni lazima tujipange vema na kuhakikisha tunashinda mechji zetu zilizobaki huku tukiwaombea mabaya wale walio juu yetu…yote kwa yote tumejipanga vema kuhakikisha malengo yanatimia,”alisema SEndeu.
Viingilio katika mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Oden Mbaga mwenye beji ya Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) vitakuwa shilingi  3,000 kwa viti vya bluu na kijani, shilingi  5,000 kwa watakaokaa viti vya rangi ya chungwa, shilingi  10,000 kwa VIP C na B na shilingi  15,000 kwa VIP A.
Mbali ya mechi ya Yanga na Villa, leo pia kutakuwa na mchezo mwingine wa ligi hiyo utakaozikuytanisha Coastal Union na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga.

Comments