YANGA IMARA HAOOO KWA WAGOSI

MABINGWA watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara kesho wataelekea jijini Tanga tayari kwa mechi yao ya ligi hiyo dhidi ya wenyeji Coastal Union 'Wagosi wa Kaya' itakayopigwa jumamosi kwenye dimba la Mkwawani mjini humo.
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema kwamba kikosi kamili cha Yanga kitakwenda huko kwa lengo la kuzoa pointi tatu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao.
"Sisi tupo kamili ndugu yangu nawashangaa hawa ndugu zetu wanahahaha mara wachezaji sijuii nini ...mpira unachezwa uwanjani na sisi tunawachezaji kibao nini hao bana,"Alisema Sendeu.

Comments