YANGA HAWATAKI KUSIKIA HABARI ZA ZAMALEK


MABINGWA watetezi wa Ligi kuu Bara Yanga wamesema wamesahau habari za yaliyotokea Cairo, Misri Jumamosi iliyopita.
Ikumbukwe kuwa Yanga siku hiyo ilitolewa na kwenye michuano la klabu bingwa Afrika na Zamalek ya huko kwa jumla ya mabao 2-1.
Ofisa habari wa Yanga Louis  Sendeu amesema kuwa amesema kuwa kukumbuka masuala ya zamalek ni sawa na kurudisha nyuma harakati zao za kutaka kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara.
Amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao katika ligi hiyo na tayari timu imeshaanza mazoezi na mambo yakienda vema kesho wataingia kambini katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya Jangwani an Twiga.
“Yaliyotokea Cairo ni sehemu ya mchezo hivyo hatuwezi kuendelea kuyawazia badala yake tunaelekeza nguvu zetu katika ligi kuu bara ili tuyweze kutetea ubingwa wetu,”Alisema Sendeu.
Yanga itashuka dimbani Jumamosi kukwaana na Azam Fc. 

Comments