SIMBA WATAKATA LIGI KUU, YANGA NAO WAJIFARIJI


Simba SC juu zaidi
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC wamejiimaarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Simba sasa wana pointi 44, baada ya kucheza mechi 20 wakati Azam ipo nafasi ya pili kwa pointi zake 41 baada ya kucheza mechi 20 pia, wakati Yanga iliyoifunga African Lyon 1-0 inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake 40, ingawa imecheza mechi 19.
Bao pekee la Simba kwenye mchezo huo, lilitiwa kimiani na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Mutesa Patrick Mafisango. Bao la Yanga lilikuwa kama la kujifunga, kwani beki Hamisi Yussuf aliokoa mpira ukambabatiza kiungo Kiggi Makassy na kutinga nyavuni.
Azam itashuka dimbani Jumapili kucheza na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam, Chamazi, siku ambayo Simba watakuwa wakimenyana na Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Jumamosi Yanga itacheza na Villa Squad Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati

Comments

  1. Dada Dina!
    Habari za Dar? mimi ni mwandishi wa habari wa siku nyingi sana...nilikuja nje kwa masomo kwa degree yangu ya kwanza ya Mass Communication na baadae Masters in Mass Communication, baadae nilipata ajira hapa Ulaya kwenye kitengo cha habari. Nipo kidogo na mshangao....nikisoma habari zako moja kwa moja naona kuwa wewe ni shabiki wa Simba...nadhani hii siyo sahihi kwetu kama waandishi kazi yetu kubwa na kuripoti na kuwa fair....naona habari uliyoandika kuwa goli la Yanga lilikuwa kama la kujifunga.....nadhani

    ReplyDelete
  2. Mdau hapo juu umenena! I was about to comment the same. Am a Tanzanian living in Beirut, Lebanon. Media and its people has to be fair but what is happening to our sister Dina is more than amazing. She is not alone there is a couple of them with no media ethics. Jaribu kubadilika dada post zako nyingi huwa huiandiki vizuri Yanga. Naelewa wewe ni Simba damu kwani hata kwenye Launching ya Simba TV ulikuwepo na timu yako ya wanazi. Acha hizo na fuata mfano kama wa Maestro, Shaffih n.k. hawa kama huwajui wezi elewa wanashabikia timu gani. Frankly speaking they are FAIR not YOU!!!

    ReplyDelete

Post a Comment