WAZEE YANGA MNASHANGAZA:TFF



RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Leodger Tenga ameshangazwa na kitendo cha wazee wa klabu ya Yanga kutoa malalamiko yao kuhusiana na adhabu walizopewa wachezaji wa timu hiyo na kusema kuwa walipaswa kukemea vitendo vya utovu wa nidhamu kwani msimamo walioutoa inaonyesha wanaunga mkono wachezaji wa Yanga.
“Utu uzima dawa si sumu…haiwezekani wachezaji watende vile halafu mzee asikemee kwani kwa kufanya hivyo inaondoa kauli mbiu ya Yanga DAIMA MBELE NYUMA MWIKO…lakini hilo halipo kwao,”Aliongeza Tenga.
Katika hatua nyinmgine, Tenga amesema kuanzia sasa uharibifu wowote utakaotokea kwenye uwanja wa Taifa klabu husika italazimika kulipa gharama ya shilinmgi milioni 10 iliyoelekezwa na Serikali.
Tenga alisema Serikali ina haki ya kutoza faini hiyo kutokana na Watanzania kushindwa kuonyesha ustaarabu wa kuuthamini uwanja huo uliojengwa na Serikali na badala yake wamekuwa wakiuharibu kutokana na vurugu zisizo na maana ambazo hufanywa na mashabiki wa baadhi ya vilabu.
“Ni sawa kwa Serikali kutangaza faini kwa uharibifu utakaotokea kwenye Uwanja wa Taifa lakini pia ifike mahali viongozi wa vilabu husika kuwaelimisha wanachama na wapenzi wao kuacha kufanya mambo yasiyo ya kistaarabu ndani ya uwanja kwani ni vigumu kwa TFF pekee kusimamia suala la ulinzi ama uangalizi wa uwanja,”alisema Tenga.
Aidha, Tenga aliongeza mpira ni burudani na furaha hivyo mambo ya kihuni yanayofanywa na baadhi ya mashabiki hayaendani na lengo la michezo na kwa mwendo huo itafikia wakati makampuni yataacha kudhamini mchezo huo na matokeo yake kuendelea kurudisha nyuma kiwango cha mchezo huo. 

Comments