WACHEZAJI YANGA MGUU NDANI, MGUU NJE

LICHA ya kamati ya nidhamu na Usuluhishi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafungulia baadhi ya wachezaji wa Yanga waliofungiwa kutokana na kumpiga mwamuzi Israel Nkongo, bado kuna uwezekano wa wachezaji hao kurejeshwa kifungoni.
Kamati ya nidhamu inayoongozwa na Kamishna mstaafu wa polisi Alfred Tibaigana ilitengua adhabu hiyo iliyotolewa na kamati ya Ligi ya TFF baada ya Yanga kukata rufaa.
Hata hivyo TFF imesema Yanga inakusanya vielezo ili kuviwasilisha kwa kamati hiyo ambayo itakutana ijumaa kwa ajili ya kulijadili suala hilo.

Comments