WACAMEROON, WAGABON WATUA BONGO KUSAKA TIMU


Mcameruni, Kengne Alain Thierry

WACHEZAJI watatu kutoka nchi za Cameroon na Gabon wapo nchini kwa ajili ya kuangalia mwenendo mzima wa soka la Tanzania kabla ya kuangalia timu watakayoweza kuichezea.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakala wa wachezaji hao Mussa Abdallah alisema wachezaji hao wapo nchini kwa siku kadhaa ambapo pamoja na mwenendo huo wanaangali hali ya hewa ya Tanzania .
Alisema nyota hao wanacheza katika klabu ya Missile Fc ambayo ilikuwa inashiriki ligi kuu ya huko iliyomalizika hivi karibuni na timu hiyo kushika nafasi ya tatu.
Aliwataja wachezaji hao ni pamoja na  washambuliaji Kengene Thiery na Nkamseu Herve Jean kutoka Cameroon na beki Moussono Charly kutoka Gabon ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon

Comments

  1. mbona kwenye habari ya sendeu anaandika habari huyo sio mchezaji huyo mwandishi wako

    ReplyDelete

Post a Comment