WABUNGE SITA KUIONGOZA SIMBA ALGERIA

                                                                                     RAGE
                                                                                 ZITTO
                                                                                    ZUNGU
                                                                          MANGUNGU
WABUNGE wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanatarajiwa kuungana na timu ya soka ya Simba kwenye mechi yake ya marudio ya kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria wiki ijayo nchini humo.
Mwenyekiti wa  Simba, Alhaj Ismail Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) alisema wabunge hao wenye mapenzi na timu hiyo wanakwenda huko kwa ajili ya kuipa sapoti timu hiyo katika mchezo huo muhimu.
Aliwataja wabunge wengine ni pamoja na Khalifa Suleiman Khalifa, Murtaza Mangungu na Zitto Kabwe , Hasnain Murji na Mussa Azzan 'Zungu'
Rage alisema kikosi chake ambacho kinatarajiwa kuondoka Jumatatu ijayo,kimejipanga vema kuhakikisha kinashinda mechi hiyo ambapo ili  iweze kusonga mbele Simba inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kushinda.Katika mechi ya awali Simba ilishinda mabao 2-0.


Comments

Post a Comment