SIKU chache
baada ya kutangazwa kwa zoezi la kusaka mwakilishi wa Tanzania kwenye
mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World 2012’, warembo 11 wamejitokeza mpaka
sasa kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo.
Mwaka huu Tanzania itatuma mwakilishi tu na si Miss Tanzania , hiyo nimetokana na mabadiliko ya
kalenda yaliyofanywa na waandaaji wa shindano la Miss World ambapo mwaka huu
fainali zake zimepangwa kufanyika mwezi Agosti 2012 nchini China .
Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu
shindano la Miss Tanzania ,
alisema kwamba zoezi hilo
linaloonekana kuvutia wengi linakwenda vema na hiyo inatokana na kasi ya
warembo kuwa juu.
Alisema
zoezi hilo litaendelea
kwa wiki kadhaa ambapo majina ya washindani hayatawekwa hadharani kabla ya
kamati kuchuja warembo wenye sifa na kubakiza kumi ambao watapanda jukwaani
katika ‘Min Miss Tanzania’ ili kumpata mwakilishi huyo.
Aidha,
Lundenga aliongeza kuwa kati ya wasichana hao hakuna hata mmoja aliyewahi
kushiriki shindano lolote la urembo licha ya warembo waliopata kushiriki Miss Tanzania hadi
hatua ya fainali (isipokuwa aliyetwaa taji) kuwa na nafasi ya kushiriki tena
ilimradi akidhi vigezo vinavyohitajika.
Wiki iliyopita
kamati hiyo ilitangaza mchakato mpya wa kumpata mwakilishi huyo ili kuendana na
kalenda ya Miss World huku mchakato wa mashindano ya Redd’s Miss Tanzania 2012
katika ngazi zote utaendelea kama kawaida na mshindi wa Redd’s Miss Tanzania
2012 atawakilisha nchi kwenye fainali za
mashindano ya urembo ya dunia mwaka 2013.
Comments
Post a Comment