VIINGILIO CHEE SIMBA V KIYOVU


WAKATI wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), Simba ikitarajiwa kurejeana na Kiyovu ya Rwanda kwenye dimba la Taifa Jumapili, kiingilo cha chini kimepangwa kuwa sh 5,000.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatika jijini Dar es Salaam jana, kiingilio hicho kitahusisha mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya bluu na kijani, ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kuhudhuria.
Taarifa hizo, zinaeleza kuwa kiingilio cha juu katika mchezo huo ni sh 30,000, ambacho kitahusisha mashabiki watakaokaa jukwaa la VIP A.
Aidha mashabiki watakaokaa viti vya rangi ya chungwa watalipa sh 8,000, VIP C sh 20,000 na VIP  B watalipa sh 15,000 .

Comments