URA WAPETA LIGI YA MABINGWA


MABINGWA wa Ugand, URA wamesonga mbele katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili baada ya miaka mitatu mfululizo ya kutolewa mapema kwenye michuano hiyo.
Alex Isabirye alifanya kazi nzuri kwenye Uwanja wa Setsoto, timu hiyo watoza kodi Uganda ikitoa sare ya bila kufungana na Lesotho Correctional Services (LSC) na kusonga mbele, baada ya awali kushinda 3-0 mjini Kampala katika mchezo wa kwanza.
Shukrani kwao, Nahodha wa URA, Manco Kaaweesa, Sula Bagala na Vincent Kayizzi, Isabirye ambao waliizima timu ya kocha Mosholi ‘Shoes’ Mokhothu.

Comments