UNGA NDO UMEMUUA WHITNEY HOUSTON


NEW YORK, Marekani
 BAADA ya kuwepo kwa hali ya utata kuhusu kifo cha mwimbaji Whitney Houston kilichotokea huko kwenye chumba alichofikia cha Hoteli ya Beverley Hills Februari ya mwaka huu taarifa kamili imeibuka na kuthibitisha kuwa mwimbaji huyo alifariki kwa sababu ya matumizi ya dawa za kulevya na ugonjwa wa moyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha upelelezi wa miili ya marehemu ilisema kwamba kuzama kwa mwili wa mwanadada huyo kulichangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuzidiwa na dawa za kulevya na ugonjwa wa moyo.
Taarifa hiyo iliendelea kupasha kuwa baada ya kufariki kwa Houston pembeni mwake kulikuwa na dawa za kulevya aina ya Xanax, Flexeril, bangi na Benadryl ambazo zimeonekana kuchangia kifo chake.
Taarifa hiyo inasema kwamba hakuna dawa aina ya cocaine iliyopatika katika chumba alichokuwa amefia mwanadada huyo.
Msemaji wa upepelezi wa kitengo hicho, Craig Harvey, alinukuliwa akisema kwamba kiasi cha cocaine kilionekana kwenye mfumo wake, kikionyesha kwamba mwanadada huyo alikuwa amekubuhu katika matumizi ya dawa hizo.

Comments